Serikali imesema kuwa itashirikiana na Kampuni ya Guru Planet kuwainua Wajasiriamali waliopo Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto wakati wa ufunguzi wa tamasha la wajasiriamali lililoandaliwa na Kampuni ya Guru Planet kwa kushirikiana na Manispaa ya Ilala ambapo zaidi ya vikundi 300 vimeshiriki.
Amesema kuwa dhumuni la Manispaa ya Ilala kufanya tamasha Kwa kushirikiana na Kampuni hiyo umetokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake za kuwajengea uwezo Wajasiriamali na kuwatafutia fursa za mitaji pamoja na masoko.
“Sisi kama Serikali tumeona kampuni hii ni mdau muhimu ambaye amewaweka Wajasiriamali kwa ukaribu na kuwawezesha kukuza utaalamu wao kila wakati, hata hivyo Manispaa Ilala imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo ili kuakikisha fursa zinapatikana,”amesema Kumbilamoto
Aidha, ametumia nafasi hiyo kuwapongeza wadau wote wa Maendeleo kwa kushirikiana na Serikali katika kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufuli kujenga dhana ya uchumi wa viwanda ili kuelekea uchumi wa kati.
-
Video: Makonda aanika ya wasanii, ‘hakuna asiyejua mmefulia’
-
Wakuu wa nchi Afrika Mashariki wakutana Arusha leo
-
Kikosi Maalum cha Polisi chatua mkoani Njombe
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Guru Planet, Nickson Martin amesema kuwa katika maonyesho hayo matarajio Wajasiriamali watajifunza na kutambua fursa mbalimbali zinazopatikana Kwa serikali Pamoja na wadau wake.