Msanii wa muziki nyimbo za asili nchini, Mrisho Mpoto ametoboa siri yake ya kuwa tofauti ya kupendelea kutembea peku jambo ambalo ni gumu kwa wasanii ambao wana majina makubwa na kioo kwa jamii.

Mrisho amesema kuwa ile tabia yake ya kutembea peku alifundishwa na Mkurugenzi wa vipindi vya Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Mpoto amesema walikaa na Ruge na kuongelea jinsi ya yeye kuwa tofauti katika mashairi yake jinsi gani anaweza kujitofautisha na wasanii wengine kama yeye.

”Ni Ruge ndio alinitengeneza mimi kuwa tofauti na mashairi yangu, mwanzoni nilikuwa naimba tu lakini baadae aliamua kunibrand na kunifanya wa tofauti”. Amesema Mrisho Mpoto.

Na sasa kuna harakati zinazoendelea juu ya kumtia moyo na kumchangia Ruge inayoenda kwa hashtag Familia ya Ruge nje ya Mutahaba, ambayo inahamasisha watu kuchanga.

Mdogo wa Ruge, Mbeki Mutahaba alipozungumza kwenye kipindi cha Clouds cha 360 alisema gharama za matibabu ya Ruge ni kubwa kuliko kawaida na hadi sasa ametumia milioni 650 na kwa siku anatumia milioni 5 au 6 kwa matibabu yake huko nchini Afika Kusini.

Katika mtandao wa kijamii wa instagram wa Mrisho Mpoto ameandika.

”Mungu ameanza kuonyesha miujiza yake sasa, nataka niwaambie kama shida ni fedha Ruge utasimama oon mchango wako kwetu ni mkubwa mno watanzania tutachangia”.

Tangu Ruge Mutahaba alazwe nchini Afrika Kusini watu mbalimbali wamejitokeza kumuongelea Ruge kwa hali chanya kuonyesha mambo ambayo amechangia katika maisha yao wakiwemo wasanii na watu wengine mbalimbali.

Aidha Ruge anasumbuliwa na tatizo la Figo na sasa yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

 

 

Video: Timaya aachia ‘Balance’ kutoka kwenye albam yake mpya
Mbunge wa Geita Mjini alilia umeme wa REA