Wauzaji na wasafirishaji nje ya Nchi viumbe pori hai wamemuomba Rais Dkt, John Magufuli awasaidie kurejesha biashara hiyo iliyositishwa miaka mitatu iliyopita, inayowasaidia kuendesha maisha yao kwasababu hawasafirishi wanyama bali ni viumbepori kama wadudu.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa chama cha wasfirishaji viumbe hai nje ya Nchi (TWEA), Adam Waryoba, amesema kuwa mwaka 2016 Serikali ilisitisha ghafla ukamataji na usafirishaji nje ya Nchi viumbe hao chini ya aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof, Jumanne Maghembe, walikuwa tayari wamesha lipa serikalini vibali vya usafirishaji.
” Miaka mitatu ya sitisho imemalizika Machi 16 mwaka huu, Mchakato wa biashara kwa mwaka unaofuata huanza Oktoba na Novemba mwaka uliotangulia, lakini wizara kupitia mamlaka ya wanyamapori, Februari Mosi mwaka huu ilitangaza leseni za biashara za mwaka huu, bila kutangaza leseni tunazofanyia biashara” alisema Waryoba.
Na kusisitiza kuwa Waziri wa sasa wa Maliasili na Utalii Dk, Hamis Kigwangalla, Mei 21 mwaka jana alilieleza Bunge kuwa Serikali itarudisha sh, milioni 173.3 walizopokea kutoka kwao lakini hadi sasa hawajafanya hivyo jambo linalopelekea wao kutojua hatima.
Biashara hiyo inahusu viumbe pori hai ambao ni Vyura. Wadudu, Mijusi, Ndege na tumbili, na ilianza kabla ya Uhuru ambapo ilifanywa na wazungu kwa wanyama.
“Baada ya Uhuru iliainishwa vyema kwa sheria ya uhifadhi wanyama pori ya mwaka 1974 na kufanya kuwa ya Watanzania wazawa” aliongeza
“Ndio maana tanamuomba Rais Magufuli atusaidie kwa sababu fedha tumelipa, viumbe pori tulikamata leseni zetu zilitoka kabla ya kusitishwa biashara hii zilikuwa 454, Tunamuomba Rais atusaidie tuendelee na biashra hii kuliko kuendelea kupata hasara na tupo tayari kukutana naye” alisema
Naye mmoja wa wafanyabiashara wa viumbe pori hai ,Deodata Nsimeta amesema sitisho hilo limewaathiri kwa sababu alikopa fedha, alikusanya viumbe pori ambao Waziri aliwaeleza kuwa atawachukua lakini hadi sasa hawajafanya hivyo, kwahiyo wanahitaji sana msaada wa Rais Magufuli.
-
Upotevu wa bilioni 5.5 bado kizungumkuti Njombe, viongozi wapingana hadharani
-
Polepole asema Maalim Seif ni fundisho