Kimbunga Idai bado ni tatizo nchini ya Msumbiji ambapo watu zaidi 1000 wameripotiwa kupoteza maisha na takribani watu 400,000 wameachwa bila makazi, huku eneo kubwa la ardhi likiwa lmefunikwa na maji.

Shirika la msalaba mwekundu limetoa tahadhari ya uwezekano mkubwa wa kutokea kwa mlipuko wa magonjwa yanayotokana na kusambaa kwa maji machafu kama vile kipindupindu kutokana na kiwango cha uchafu ulioingia kwenye vyanzo vya maji.

Aidha Serikali ya Msumbiji imesema kuwa watu 84 wamefariki na wengine takribani 100,000 wanahitaji kuokolewa kwa dharura karibu na mji wa Beira.

Hata hivyo Kimbunga Idai kilishuka katika mji wa bandari wa Beira siku ya Alhamisi kikiwa na upepo wenye kasi ya hadi kilomita 177 kwa saa, lakini mashirika ya misaada yalifika katika eneo hilo siku ya Jumapili.

Magari mengi ya misaada yamekwama katika barabara zilizofungwa na maji na yameshindwa kufika katika maeneo yanakoelekea, ambapo hali hiyo imesababisha kusimama kwa shughuli zao pia.

Taasisi ya kitaifa ya kupambana na majanga nchini Msumbiji imezipokea familia 3,800 katika jimbo la Sofala, huku mashirika kadhaa ya misaada yanasaidia jitihada za serikali katika kuwatafuta na kuwaokoa watu amabo wapo kwenye maji na kutoa misaada ya chakula.

 

 

Mama aichoma na maji ya moto mikono ya mwanae
Theresa May mambo bado magumu, ajipanga kutuma maombi Umoja wa Ulaya