Mkuu wa Wilaya Kisarawe, Jokate Mwagelo jana aliandaa hafla maalumu kwa ajili ya harambee ya kutokomeza zero kwa wasichana wa kisarawe ambapo watu maarufu na viongozi walihudhuria na kutoa ahadi kede wa kede kukamilisha jambo hilo.
Mapema leo kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram wa Mhe.Mwagelo amempa shavu nono Piere maarufu kwa usemi wa “Utabaki kuwa juu, utabaki kileleni”, aliyejipatia umaarufu kwa usemi huo.
Jokate amempa shavu hilo mara baada ya kugundua ujuzi wake wa ufundi mbao na kumtaka wafanye kazi pamoja katika kutengeneza madiwati ya shule ya sekondari kisarawe inayotarajiwa kujengwa hivi karibuni.
Aidha wakati hafla hiyo inaendelea, Mkuu wa mkoa Dar es salaam, Paul Makonda amekemea vikali namna ambavyo makampuni makubwa yanamtumia piere kama balozi ambaye anavaa uhusika wa ulevi na kudai kuwa hawajengi taifa la kesho zaidi ya kulibomoa.
Hivyo Mhe.Jokate kupitia ukurasa wake umemuomba radhi Piere kwa usumbufu ulijitokeza na kumfanya akwazike kwa namna moja au nyingine.
Kupitia ukurasa wake ameandika.
“Samahani kwa kukwazika lakini tunashukuru kwa kushuriki Tokomeza zero Kisarawe, Elimu itabaki kuwa juu, juu kileleni” Jokate.
Aidha mbali na shavu hilo katika hafla hiyo Piere aliweza kuchangia shilingi laki 1 kutokomeza Zero Kisarawe, ambapo jokate ametambua mchango huo na kutanguliza shukrani zake kubwa.