Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip mpango amesema kuwa serikali imewatahadharisha wananchi kutoshiriki kwenye biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kwa njia sizizo halali.
Ameyasema hayo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa hivi sasa kuna taarifa kuwa kuna baadhi ya maeneo ya mipakani na kwenye majiji ya Dar es salaam na Arusha wamejitokeza watu wanaofanya biashara haramu ya kubadilisha fedha za kigeni ambao wameathiri baadhi ya wananchi kwa wizi.
Amesema kuwa serikali katika kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kuwa sekta ya fedha inachangia ipasavyo utulivu na ukuaji wa uchumi nchini ambapo Benki kuu ya Tanzania ilibaini uwepo wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni ambayo yalikuwa yakiendeshwa pasipo kuzingatia sheria ya foreign exchange act 1992 ,kanuni za the foreign exchange (bureau de change) regulations 2015 na marekebisho ya mwaka 2017 na taratibu za utoaji wa huduma za ubadhilishaji wa fedha za kigeni.
Aidha, katika hatua nyingine amesema zoezi hilo lilibaini pia uondoshwaji wa fedha katika mfumo rasmi wa fedha na kuelekezwa kwenye mifumo ya utakatishaji wa fedha haramu kupokea amana kutoka kwa wafanyabiashara kinyume cha matakwa ya leseni za biashara husika, kudhoofika thamani ya shilingi, pamoja na mambo mengine ambayo yalianza kuathiri usalama wa nchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga amesema kuwa maduka mengi yalihusika katika utakatishaji wa fedha kwani zoezi hilo kwa Dar es salaam lilihusisha maduka 87 katika maduka 87 maduka 5 hayakukutwa na ukiukwaji mkubwa na maduka 82 yalikutwa na viashiria kuwa yalihusika katika .
Hata hivyo ameongeza kuwa serikali kupitia benki kuu ya Tanzania inawataka wafanyabiashara ya huduma ya kubadilisha fedha za kigeni kuzingatia na kutii sheria ya foreign exchange 1992 ,kanuni ya foreign exchange (bureau de change) regulations 2015 na marekebisho ya mwaka 2017,masharti ya biashara ya huduma ya kubadilisha fedha za kigeni na maelekezo ya msingi (B.O.T) wa sekta ya fedha Nchini.