Leo April 10, 2019 Tovuti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imechapisha na kuwasilisha Ripoti Kuu ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Juu ya Taarifaza Fedha za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Katika ripoti yake ameyataja mashirika ya umma ambayo yana uhaba kifedha na kujiendesha kwa hasara kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.
”Katika ukaguzi wetu tumebaini mashirika 14 yenye matatizo makubwa ya kifedha hadi kupata hasara hadi kusababisha madeni kuwa makubwa zaidi ya mahitaji yao katika mashirika hayo mashirika 11 yana ukwasi hasi, na kwa maana hiyo kuna mengine yamekuw ayanajiendesha kihasara kwa zaidi ya miaka miwili, kufuatia hali hii mashirika haya tumeona kwamba hayawezi kujiendesha bil akutegemea msaada wa kiserikali kuu, hivyo ipo hatari kubwa ya kushibndwa kendelea kutoa huduma kwa jamii”. Amesema CAG.
Ametaja mashirika hayo ya umma yenye hali mbaya kifedha.
- Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
- Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL)
- Mamlaka ya maji safi
- Usafi wa Mazingira Lindi
- Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC)
- Bodi ya Utalii Tanzia
- Shirika la Maji Safi Dar esa salaam (DAWASCO)
- Kampuni ya Maendeleo ya Nishati Joto (TGDC)
- Baraza la Taifa la Biashara
- Mamlaka ya Maji Safi Mtwara na Mwanza
- DAWASA
- Kampuni ya Usafirishaji ujenzi na ukarabati wa Umeme (TANESCO)
- TTCL – Pesa
- Bodi ya maziwa Tanzania