Leo Mei 12, 2019 ni siku ambayo duniani kote tunawakumbuka na kuwa enzi mama zetu. Kwa mara ya kwanza siku hii iliadhimishwa mwaka 1908.
Sote tumezaliwa na mama zetu, hata kama wapo wachache ambao kwa bahati mbaya, kwa sababu hii au ile hawakuwahi kuonja upendo na mahangaiko ya mama zao, lakini ukweli ni kwamba yako mambo ambayo bila mama zetu yasingefanyika, na kubwa katika hayo ni kutubeba tumboni hadi tukafikia umri wa kuwa tayari kuwa hai bila kuwa matumboni mwao.
Siku hii inamkumbusha kila mmoja wajibu wake kwa mama yake, kwa wale ambao mama zao wametangulia mbele za haki, huitumia siku hii kuiwaombea na kuwashukuru kwa kujitoa kwao kuwalea watoto wao.
Mama ni mwalimu mkuu katika makuzi ya mtoto, wakati mama akifanya hayo yote kwa ajili ya kutengeneza maisha yangu niliyonayo sasa kwa kujinyima mimi nile, hakuvaa, mimi nipendeze, hakulala, mimi nipate usingizi, wapo baadhi ya watoto wakishakua na kuanza kujitegemea huwa wanamsahau mama.
Upo usemi kuwa mama anaweza kuwa na watoto wanane, akawalea na kuwasomesha wote kwa usawa lakini anapozeeka, watoto wale hushindwa kumtunza mama yao vile inavyostahili huku kila mmoja akimtegea mwenzake.
Tunapaswa kuadhimisha siku hii kwa kujiuliza maswali! Umemfanyia nini mama yako, yupo wapi na je? anapata mahitaji muhimu wakati huu ambao wewe umeanza kujitegemea?
Lazima kila mmoja ahakikishe siku zote mama yake anapata mahitaji muhimu. Na zaidi ya kumpa zawadi na mahitaji mengine, hata kumjulia hali ni sehemu ya kumtunza.
Malezi yanaweza kufanywa na mtu yeyote mwenye mapenzi mema, lakini “role” ya mama (mzazi au mlezi) kwa mtoto ni “indisputable”.
Naomba wana Dar24 tuungane:
- Kuwapongeza mama zetu na walezi wote.
- Kuwaombea pumziko la Amani mama waliotangulia.
- Kuwatia moyo mabinti wanaoogopa majukumu ya kuwa “mama”.
- Kuwasamehe wakina mama waliofanya makossa makubwa ya umama kwa watoto wao.
- Kulaani vitendo vilivyo kinyume na hurka sahihi ya umama kama utoaji mimba, kutupa na kutelekeza watoto.
- Kulaani wakina baba wanaowatesa, kuwatumikisha na kuwatelekeza mama wa watoto wao.
- Kulaani watoto waliowatelekeza wazazi wao, hasa mama zao.