Dar24 Media inapenda kuwatangazia nafasi za kazi ya uandishi wa habari na utangazaji katika vipengele vifuatavyo:
- Burudani
- Michezo
- Siasa
- Uchumi
Mwombaji awe sifa zifuatazo:
Awe na Shahada (Degree) ya Uandishi wa Habari/Utangazaji au Stashahada (Diploma) ya Uandishi wa Habari/Utangazaji.
Pia, awe mbunifu na mwenye kipaji cha utangazaji.
Mwenye sifa hizo afike katika ofisi za Dar24 Media zilizopo ndani ya Jengo la Ofisi za Data Vision International, Mikocheni Jijini Dar es Salaam, barabara ya Rose Garden, mtaa wa Mikumi, siku ya Jumamosi, Mei 18, 2019 kuanzia saa 4:00 Asubuhi kwa ajili ya usaili.
Muombaji aje na nakala zilizothibitishwa (certified copies) za cheti cha kuzaliwa na vyeti vya taaluma tajwa.
Kwa mawasiliano: news@dar24.com