Homa ya Dengue maarufu kama homa ya kuvunja mifupa ni homa iliyokamata maeneo mbalimbali ya mji wa Dar es salaam, ikiwemo Masaki na Tandale hivyo ni vizuri watanzania kufahamu undani wa ugonjwa huu.
Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba ya moja kwa moja, ila kwenye kipindi cha Afya Tips, Daktari wa magonjwa ya binadamu, Emmanuel Mwakasumi ameeleza kwa kina sababu ya tiba ya ugonjwa wa Dengue kuwa ni maji pamoja na dawa za kutuliza maumivu aina ya Panadol.
Zipo dawa nyingi za kutuliza maumivu zikiwemo Diclofenac, Dicloper na kadhalika, lakini maumivu ya ugonjwa wa Dengue hayapaswi kutibiwa na dawa aina ya Declofenac.
Daktari amefafanua vizuri zaidi kwenye video hapa chini, kwa nini maji, panadol na si Diclofenac
Japokuwa Diclofenac ni dawa iliyosajiliwa na mamlaka ya chakula na dawa TFDA, kwa matumizi ya kutuliza maumivu na kuondoa uvimbe unaosababishwa na magonjwa mbalimbali.
Pamoja na kazi kubwa ya Diclofenac kwenye mwili wa binadamu, TFDA imetaja baadhi ya madhara yatokanayo na dawa iyo endapo itatumika kwa wingi na kutaja kuwa husababisha vidonda vya tumbo, kuharisha, kutapika, na mwili kuwasha.
Hivyo Mamlaka ya udhibiti wa Dawa ya nchi za umoja za Umoja wa Ulaya (European Medicines Agency yenye makao yake makao makuu London, Uingereza Imetoa tahadhari kwamba watu wenye matatizo ya moyo, na wanaovuta sigara wanaweza kupata matatizo kwenye moyo na mfumo wa damu ikiwa watatumia Diclofenac kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu.
Vivyo hivyo wagonjwa wa Dengue hawapaswi kutuliza maumivu ya ugonjwa huo kwa dawa za Diclofenac.