Pweza ni moja ya samaki wanaopatikana baharini ambao wamepata umaarufu mkubwa baada ya tafiti kubainisha kuwa wanaongeza nguvu za kiume kwa waliopungukiwa.
Samaki huyu hana umbo la kutamaniwa kuliwa ndiyo maana baadhi ya watu wa bara wanapotembelea mikoa ya Pwani na kukuta wengi wakikimbilia kumla.
Licha ya kuongeza nguvu za kiume, virutubisho vinavyopatikana katika pweza vinasaidia kumkinga mlaji na saratani ya mdomo, utumbo mkubwa, tumbo, matiti na shingo ya kizazi.
Aidha virutubisho hivyo vinachochea hamu ya mlaji kufanya tendo la ndoa hii baada ya kuwa na wingi wa protini na madini ya selenium.
Kwa mwenye tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa ni vema akaweka utaratibu wa kula pweza na supu yake japo kwa wiki mara mbili.
Kwa upande wa kinamama wanaonyonyesha, kula pweza kunasaidia kuzalisha maziwa ya kutosha kwa watoto wao.
Supu ya pweza nayo ni nzuri inaongeza madini joto mwilini na kupunguza athari ya maradhi ya moyo kutokana na virutubisho vilivyomo ndani ya samaki huyo.
Kula pweza kwa wingi ili kuweza kujipatia faida lukuki katika afya yako.