Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Zanzibar ZFA, Seif Kombo Pandu, ameeleza kupokea kwa masikitiko msiba wa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Zanzibar Ibrahim Jeba.
Pandu amesema Jeba amefarikiĀ Septemba 18, 2019, katika Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar na wanaendelea na taratibu za mazishi kwa kushirikiana na familia.
”Ni kweli amefariki, chanzo bado hakijajulikana kwa mujibu wa madaktari lakini tu kuna tetesi kuwa alikuwa na matatizo ya ini ambapo klabu ya Azam ilisimamia kiasi matibabu yake na kushauri aachane na soka”, amesema Pandu.
Kiungo huyo wa zamani wa vilabu vya Azam na Mtibwa Sugar mpaka mauti yanamkuta, alikuwa mchezaji wa Chuoni FC ya Zanzibar.