Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo na tahadhari ya siku 5 ya kuwepo kwa vipindi vifupi vya mvua nyingi katika mikoa ya ukanda wa Pwani, Visiwani Zanzibar na Kusini mwa Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jana Oktoba 8, 2019 na Mamlaka hiyo, Imeonesha kuwa leo Jumatano Oktoba 9, Kwa mikoa ya Dar, Tanga, Pemba, Unguja na Kaskazini mwa Morogoro kutakuwa na mvua kali.
TMA pia imetoa angalizo kwa wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kusema kuwa kutakuwa na upepo na mawimbi makubwa.
Athari zinazoweza kujitokeza ni ndogo zikiwemo za kuchelewa kwa watu kufika makazini, Na kuathirika kwa shughuli za uvuvi kwa ukanda wa Pwani, lakini pia baadhi ya shughuli kusimama.
Tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa na mawimbi makubwa imetolewa kwa siku 5 kuanzia jana Oktoba 8, 2019.