Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo Desemba 27, 2019 amefanya usajili wa laini yake ya simu kwa kutumia alama za vidole na kuwasisitiza watanzania wote kuhakikisha laini zao za simu zinasajiliwa kama ilivyoelekezwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA).
Rais Magufuli amefanya usajili huo Chato mjini mkoani Geita na kutangaza ongezeko la siku 20 kuanzia januari mosi hadi januari 20, 2020 ili kwa wale ambao walikosa nafasi ya kusajili katika kipindi cha awali kilichowekwa na TCRA, kwa sababu mbalimbali wakamilishe usajili.
Amesisitiza kuwa baada ya muda huo hakuna kisingizio chochote kitakacho kubalika na ameagiza TCRA kuhakikisha laini ambazo hazijasajiliwa zinazimwa kama ilivyopangwa,…Bofya hapa kutazama.