Daktari wa hospitali binafsi ya Dental Clinic iliyopo Sinza Mori Jijini Dar es salaam, Awadhi Juma (40), na muuguzi Kidawa Ramadhani, wamefikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka saba, likiwemo la kutoa mimba wanawake na kutakatisha fedha kiasi cha Tsh. 260,000/=.
Washtakiwa hao wamefikishwa Mahakamani jana na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu mkazi, Vicky Mwaikambo.
Kabla ya kusomewa mashtaka yao, Hakimu Mwaikambo alisema washtakiwa hao hawatakiwi kujibu chochote kwakuwa Mahakama ya Kisutu haina uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa DPP.
Akiwasomea hati ya mashtaka, wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon pamoja na Glory Mwenda, alidai kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 139/2019.
Wameeleza kuwa katika tarehe tofauti Oktoba 2019 eneo la Sinza Mori, washtakiwa hao wakiwa na lengo la kutoa mimba waliingiza bomba la sindano katika uke wa mwanamke aina za F.R na S.S na kusababisha kuharibika kwa mimba.
Katika shtaka jingine, imeelezwa kuwa katika tarehe tifauti, Agosti 2002, Jijini Dar es salaam, mshatakiwa Juma kwa lengo la kudanganya alighushi cheti cha Diploma cha utaalamu wa tiba ya kinywa akionyesha ni halali na kimetolewa na chuo cha tiba cha Muhimbili wakati akijua si kweli.
Shtaka la nne, wakili Mwenda alidai kuwa Februali 20, 2015 Jijini Dar es salaam, Juma alighushi leseni ya biashara ya tarehe hiyo akionesha imetolewa na manispaa ya kinondoni wakati akijua si kweli.
Katika shataka la kutakatisha fedha, Juma anadaiwa kati ya Mei 2015 na Desemba 4, 2019 alijipatia Tsh 260,000/= wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la jinai la kughushi.
Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na Hakimu aliahirisha hadi Januari 10, 2020 itakapotajwa.
Washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.