Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imezipiga faini kampuni za simu za baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya leseni na kukidhi viwango vya ubora wa huduma kwa mujibu wa Kanuni za Ubora wa Huduma za mwaka 2018.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Utekelezaji wa Sheria wa TCRA, Dkt. Philip Filikunjombe amezitaja kampuni hizo kuwa ni Airtel Tsh. Bilioni 1.6, TTCL Tsh. bilioni 1.6, Viettel (Halotel) Tsh. milioni 900, Zanzibar Telecom Tsh. milioni 850, Tigo Tsh. milioni 500 na Vodacom Tsh. milioni 450.
Kwa mujibu wa taarifa ya upimaji wa ubora wa huduma kati ya Julai, Agosti na Septemba 2019, imebainika kampuni hizo zimeshindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya ubora wa huduma kinyume na matakwa ya Kanuni za Ubora wa Huduma, 2018.