Mfanyabiashara wa Ng’ombe minadani mkazi wa kijji cha Irisya mkoani Singida, Imanuel Njou (37) ameuawa kikatili kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali na kisha mwili wake kufungwa kwenye sandarusi na kufukiwa kwenye shimo la choo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na watu wa karibu, Marehemu alipigiwa simu kwenda kununua Ng’ombe kwa mtuhumiwa ambaye haijulikani nini kilitokea ila alimgeuka na kumuua kisha kuchukua fedha zake, na kumfukia kwenye shimo la choo chake.

kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya kufanya tukio hilo alienda kwa mganga wa kienyeji mkoani Manyara kuoshwa kwa dawa ya kuondoa mikosi ili balaa hilo limpitie mbali na asikamatwe na polisi, lakini Mganga huyo alimsaliti na kutoataarifa polisi.

Mganga huyo awali aliahidi kumsaidia madawa ya kumuosha na nyingine ya kuweka kaburini, hivyo waliondoka hadi Irisya kutoka Manyara ali wakakamilishe dawa.

Mtuhumiwa alipofika nyumbani akiwa na mganga wake alionesha mahali alipotupa mwili wa marehemu na mganga aliondoka hadi kituo cha polisi Singida na kutoa taarifa hizo za mauaji, polisi wakamkamata mara moja mtuhumiwa.

Timu ya madaktari kutoka kituo cha Afya Sepuka walifukua shimo hilo na kukuta mwili wa marehemu Imanuel Njou ukiwa katika mifuko miwili ya sandarusi

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa awali baba yake mtuhumiwa alimuuliza sababu za kufunika choo chake wakati bado kipya hakijatumika muda mrefu na kujibiwa kwamba alimuona nyoka ameingia kwenye shimo hilo la choo, na alipotaka kumuua simuyake ilitumbukia.

Kamanda wa Polisi mkoani Singida, ACP Sweetbert Njewike, amewaambia waandishi wa habari kuwa Njou alipotea Oktoba mwaka huu na hawakupata taarifa yeyote hadi Desemba 22 walipogundua ameuawa na kufukiwa kwenye shimo la choo.

Amesema hadi sasa wanawashikilia watu watatu ili kubaini chanzo cha mauaji hayo, ambao ni Bashiri Hamisi, Hamisi Salumu na Hamida Hamisi.

Tanga wapewa DK. 30 kusherehekea mwaka mpya
Video: Chadema kuipinga sheria ya utakatishaji fedha, 2019 yaondoka na kumbukumbu nzito