Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mwalimu Arnord Exaud Mlay (30), kwa tuhuma za kuwalawiti watoto watano wenye umri kati ya miaka 10 hadi 16 na kutoa nafasi kwa wazazi wengine ambao watoto wao wamefanyiwa ukatili wa aina hiyo kuendelea kufikisha taarifa polisi.

Mwalimu Mlay ambaye ni mkazi wa Semtema ni mwalimu wa kujitolea kwenye shule moja mkoani Iringa, anatuhumiwa kulawiti watoto watano wakiwemo wanne wa shule ya msingi na mmoja wa shule ya sekondari aliokuwa akiwafundisha masomo ya ziada nyumbani kwake (tuisheni).

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, ACP Reinada Milanzi amesema kuwa kwa mujibu wa upelelezi mtuhumiwa akiwa nyumbani kwake kwa nyakati tofauti aliwalawiti watoto hao.

Amesema kwa mara ya mwisho alimlawiti mwanafunzi Desemba 12 mwaka huu na alikamatwa Desemba 15 mwaka huu saa nne asubuhi nyumbani kwake mara baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema na wazazi wa watoto hao.

Moja ya tukio la ulawiti ambalo mtuhumiwa amelifanya ni kuanzia mwaka 2016 ambapo alianza kumlawiti mtoto wa miaka 15 kwa kumpaka mafuta ya vilaninishi nyuma ya maumbile na kumuingilia kimwili huku akitishia kumuua endapo atatoa siri hiyo kwa wazazi na jamii.

ACP Reinada amesema mtoto huyo baada ya kuona vitendo hivyo vimekithiri aliamua kuwaandikia wazazi wake barua akiwajulisha kwamba hataweza kwenda tuisheni ya jioni kwa sababu ya kuchoshwa na vitendo hivyo vya kikatili na endapo hawata ridhia atajiua.

kwa mujibu wa taarifa za polisi bado mtuhumiwa huyo hajafikishwa Mahakamani kama habari zinavyosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinazoeleza kuwa amehukumiwa kifungo cha maisha na viboko 50.

Bashiru afunguka alivyouza gulioni " Shahada ya chuo haimaanishi kupata fedha"
Tanga wapewa DK. 30 kusherehekea mwaka mpya