Hofu imeathiri watu wengi Duniani katika maisha yao kwa namna moja au nyingine. hofu hizi zinaweza kusababishwa na mazingira, mtu, kitu au sababu za kisaikolojia.
Inaelezwa kuwa hofu isiposhughulikiwa kwenye maisha inaweza kuwa ni kikwazo kikubwa cha mafanikio ya mtu kwani wengi hutamani kukabiliana na hofu lakini bado hawajui njia za kutumia, kwa kufanya mabo haya matatu unaweza kukabiliana nayo kwa urahisi.
1: Kizoee kile kinachokupa hofu
Hii ni kwasababu kukimbia kile kinachokuogopesha hakuwi suluhisho la hofu yako bali huifanya iimarike zaidi. Mfano unaogopa kukaa juu ya ghorofa refu anza taratibu kukaa kwa muda mchache mara kwa mara hadi pale utakapo zoea.
Kwa njia hii baada ya muda utaweza kukizoea kile kinachokutisha na hautakuwa na hofu tena juu yake.
2: Punguza au ondoa mawazo na imani potofu
wakati mwingine watu wanapata hofu kutokana na imani au fikra potofu pekee. kwamfano unaogopa kenge kwakuwa umesikia akikupiga na mkia wake pindi atakapo kufa na wewe utakufa, je? una uhakika wa kisayansi juu ya hilo?
Maswala mengi yanayowaogopesha watu ni kutokana na imani potofu na wala hakuna ukweli wowote.
Hivyo basi jitahidi kuchunguza kama kweli linalokupa hofu ni kweli au ni fikra na imani potofu tu.
3: Tafakari madhara ya hofu
Hebu fikiri jinsi hofu itakavyoathiri ufanisi na utendaji kazi wako, usikubali hofu ionekane kubwa kuliko madhara yake.
Kama hofu inakuzuia kufanya kazi kwa ufanisi ule unaotakiwa, kwanini ikutawale? kwa mfano ukiwa unahofu ya mitihani, umesha wahi kufikiri jinsi hofu hiyo itakavyokuathiri katika mitihani yako kuliko hata kilichokuwa kinakutisha kwenye mitihani yenyewe?
Anza kuwaza tofauti sasa, usikubali hofu ikutawale kuliko athari zake. Ukizingatia hili hautaogopa tena hofu bali utaiepuka.