Mbali na kulika kama tunda, ndizi zina manufaa mengine hasa katika urembo wa ngozi, ndizi zina virutubisho muhimu vinavyoboresha ngozi ndizi zina aina tatu za sukari zinzojulikana kama ‘sucrose’ ,’fractose’ na ‘glucose’. fahamu matumizi ya ndizi katika urembo.
Ndizi husaidia kuondoa chunusi, changanya asali na ndizi moja iliyopondwa na upake kwenye uso na shingo nawa uso na maji ya fufutende baada ya muda wa nusu saa.
Kungarisha uso, ndizi huwa na vitamini C ambavyo husaidia kuweka ngozi kuonekana iking’aa, kwenye ndizi iliyopondwa ongeza vijiko vidogo viwili vya juisi ya limau na upake kwenye uso na shingo osha na maji ya fufutende baada ya dakika 20 ni vizuri kupaka mchanganyiko huu wakati unapoenda kulala.
Kuzuia mikunjo, ponda parachichi na ndizi pamoja mchanganyiko huu hulainisha ngozi ya uso na kuwa laini lakini pia upunguza ukubwa wa matundu ya ngozi ya uso wako.
Kusugulia uso (Scrubing) unaweza ukachanganya ndizi na sukari kijiko kimoja kisha paka usoni na usugue taratibu, ndizi hulainisha ngozi kavu na sukari huondoa seli zilizokufa kwenye ngozi.