Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Dkt. George Msasi amesema kuwa wastani wa watoto watatu hadi watano wilayani humo huungua kwa moto au maji ya moto.
Dkt. Msasi amesema kuwa watoto ndiyo wamekuwa waathirika wakubwa wa ajiali za moto na maji yaliyochemka kutokana na kuwekwa sehemu ambazo si salama.
Ameeleza kuwa baadhi ya wazazi ni wazembe katika ulinzi wa watoto kwani huweka majiko kwenye maeneo hatari kwa watoto, chai au uji sehemu ambazo watoto wanaweza kufikia kwa urahisi na kuungua.
” Kwa siku ni watoto watatu hadi watano wanaoletwa hospitalini hapa kutibiwa na kulazwa wakiwa na majereha ya kuungua na moto au maji ya moto ambayo wazazi walikuwa wakichemsha na wengine wakiweka majiko maeneo hatarishi kwa watoto” amesmea Dkt. Msasi
Hata hivyo amebainisha huduma ya awali ambayo watoto hupatiwa ni kuongezwa damu haraka ili wasipoteze maisha kwakuwa kitaalamu seli za mwili zikisha ungua kutokana na moto husabibisha damu kupungua kwa wingi mwilini. na ametoa wito kwa wazazi kuwa waangalifu.