(Picha kwa hisani ya Mwananchi)

Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewasili katika ofisi za Makao makuu ya CCM Jijini Dodoma ikiwa ameitikiwa wito aliopewa na chama hicho kwa ajili ya kuhojiwa na Kamati ya Udhibiti na Maadili.

Membe amewasili leo Alhamisi, Februari 6, 2020, saa 3:15 asubuhi kwa gari aina ya Range Rover yenye namba T 748 CNV na kupokelewa na maafisa wa chama hicho.

Membe ni miongoni mwa vigogo watatu wa chama hicho watakaohojiwa, wengine ni Makatibu Wakuu wastaafu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, wakituhumiwa kuwa na mienendo isiyofaa.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuvuja kwa sauti za mawasiliano yao kwa njia ya simu, wakizungumza kwa mtazamo hasi kuhusu uongozi wa chama hicho na mpasuko.

Aidha, uamuzi wa kuwaita na kuwahoji makada hao waandamizi wa CCM ulipitishwa na vikao vya CCM vilivyofanyika Desemba 13, mwaka jana Jijini Mwanza.

 

Eric Abidal anusuru kibarua chake FC Barcelona
Lil Wayne ahisi ni raia wa Nigeria, adai ‘mimi na mama inabidi tujadili’