Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi amewataka raia wa nchi hiyo kuwa watulivu na wavumilivu, baada ya kutokea mauaji katika mji mkuu wa nchi hiyo, New Delhi, yaliyosababisha vifo vya watu 21.
Mauji hayo yalitokea baada ya waumini wa dini ya Kihindu na Kiislamu kupambana mjini Delhi, chanzo kikiwa ni mabadiliko yaliyofanywa na bunge la nchi hiyo ya kuridhia wahamiaji kupatiwa uraia.
Awali mabunge yote mawili ya India yalipitisha muswada ulioridhia kuwa na sheria wa kuwaruhusu wakimbizi kutoka katika mataifa mengine kupatiwa uraia wanapokuwa wamekabiliwa na mateso ya kidini, lakini muswada huo ukiwabagua Waislamu.
Hali hiyo ilisababisha maandamano makubwa nchini India kwa siku kadhaa na baadaye mahakama iliingilia kati baada ya shauri hilo kufikishwa makahamani.
Mahakama Kuu ya India iliamuru serikali ya nchi hiyo kupitia tena miswada hiyo ambayo ilionekana kuwa na utata.