Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, George Simbachawene amepiga marufuku ukamataji wa wananchi na madereva bodaboda na kufanya operesheni ya aina yoyote kwa kukurupuka bila kufuata utaratibu, akieleza kuwa vitendo hivyo vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani badala ya kujenga amani.

Ameagiza kila operesheni itakayopangwa kufanywa na Jashi la polisi nchini, inapaswa kutolewa taarifa kwa mkuu wa wilaya ili ajue nini kitafanyika kwa kuwa yeye ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya.

Akizungumza katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama cha wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Simbachawene amesema ukamataji usio na mpangilio hauna tija na unaweza kuvunja amani badala ya kujenga amani.

” Wananchi wanawalalamikia askari wetu sana kakamata bodaboda bila sababu, siyo bodaboda tu, hata kukamata kamata ovyo watu, ukamataji mwingine unakuwa kama kukomoa, hauna tija, hauleti amani badala yake unasababisha amani itoweke” Amesema Simbachawene.

Amesema vyombo vya ulinzi na usalama ni vya wananchi, na operesheni yoyote haipaswi kufanyika bila mkuu wa wilaya kupewa taarifa. Ndiyo utaratibu unapaswa kuwa hivyo.

 

Serikali: Msikumbatiane kuepuka Corona, Biashara zifanywe mtandaoni
Askari wasio na mafunzo kusimamishwa kazi