Mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amemkaribisha aliyekuwa Waziri wa mambo ya nje na aliyefukuzwa uanachama CCM, Bernad Membe katika chama chao.
Lipumba amesema chama hicho wanatarajia kusimamisha mgombea wa Urais wa Jamhuri na wa Zanzibar pamoja na wabunge na madiwani na amebainisha nafasi ya Membe kujiunga na chama hicho.
Amesema Membe sasa ana uhuru wa kujiunga na chama chochote cha kisiasa na akitaka kujiunga CUF si lazima kwenda kwake, bali anaweza kwenda tawi lolote la CUF kuchukua kadi na kujiunga.
Profesa Lipumba alibainisha hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa ndani wa viongozi wa chama hicho wilayani Morogoro uliofanyika jana alipokuwa akihitimisha ziara yake kwenye wilaya za mkoa wa Morogoro iliyolenga kuimarisha uhai wa chama hicho.
Amesisitiza kuwa CUF bado inaungwa mkono na wananchi wa Zanzibar hivyo wanaimani ya kufanya vizuri na sera zao si za kususia uchaguzi kwani kususa ni sawa na kuacha kulinda shamba la mihogo