Marekani na kundi la wanamgambo wa Taliban wametia saini makubaliano ya amani yanayolenga kumaliza vita vya miaka 18 nchini Afghansitan na kuwezesha Marekani kuondoa wanajeshi wake nchini humo.
Wakati wa hafla ya kuyatia saini makubaliano hayo iliyofanyika mjini Doha, Qatar, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Mike Pompeo ametoa wito kwa Taliban kuheshimu ahadi ilizotoa ikiwa ni pamoja na kukomesha mahusiano yake na makundi ya itikadi kali.
Chini ya mkataba huo Marekani itaanza kuondoa wanajeshi wake kwa makubaliano ya Taliban kuzuia mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Afghanistan.
Pindi kundi la Taliban litakapotimiza masharti ya mkataba huo Marekani itaondoka wanajeshi wake wote ndani ya muda wa miezi 14 inayokuja Kutiwa saini mkataba huo kunatimiza moja ya ahadi muhimu ya wakati wa uchaguzi iliyotolewa na rais Donald Trump ya kuindoa Marekani kutoka vita visivyokwisha ikiwemo nchini Afghanistan.