Katika kuzuia kuenea zaidi kwa virusi vya Corona, Italia imetangaza kufunga shule zote na vyuo vyote hadi Machi 15, 2020 huku Mtandao wa Facebook ukitangaza kufunga ofisi zake za Seattle kwa wiki moja baada ya Mfanyakazi mmoja kupata virusi hivyo.

Idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi vya Corona ulimwenguni imefikia 3,286, idadi ya Wagonjwa 95, 483 huku idadi ya Watu waliopona ikifikia 53,688. China pekee ina Wagonjwa 80,430 na vifo 3,013.

Nje ya Ardhi Kuu ya China, vifo vingi vya ugonjwa huu vimetokea Italia vifo 107, Iran ina vifo 92, Korea Kusini ina vifo 35 na Marekani vifo 11.

watu 1,000 Jijini Yew York wameshauriwa kujiweka karantini huku mamlaka zikiendelea kutafuta walioathirika, Shule ya Mount Vernon imefungwa hadi Machi 9 huku chuo cha ‘The Lake Washington Institute of Technology’ huko Washington nacho kikifungwa.

Marekani yatia doa makubaliano ya amani na Taliban
Live: Makamu wa rais akifungua mkutano wa mawaziri wa kazi na Ajira SADC