Serikali nchini China imepiga marufuku ulaji na ufugaji wa wanyama wa Porini nchini humo kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona ikiwa inaaminika kuwa vilianzia kwenye soko la wanyamapori katika mji wa Wuhan.

Ingawa haijulikani ni mnyama gani aliyeambukiza virusi hivyo kwa Binadamu ila Popo, Nyoka na Kakakuona wanahisiwa. China imekiri kuhitaji kudhibiti sekta ya Wanyamapori.

Virusi hivyo vimeendelea kusambaa Ulimwenguni ambapo hadi sasa vimethibitika katika Mataifa 85, Mataifa 7 ni ya Afrika (Algeria, Misri, Nigeria, Senegal, Afrika Kusini, Morocco na Tunisia).

Idadi ya watu waliofariki kutokana na Virusi vya Corona Ulimwenguni imefikia 3,387, idadi ya Wagonjwa 98, 436 huku idadi ya Watu waliopona ikifikia 55,659. Ardhi China pekee ina Wagonjwa 80,555 na vifo 3,042.

Hadi mapema leo, nje ya Ardhi ya China, vifo vingi vya ugonjwa huu vimetokea Italia kwenye vifo 148, Iran yenye vifo 108, Korea Kusini yenye vifo 40 na Marekani yenye vifo 14.

Serikali yakanusha " Zanzibar hamna Corona"
Pwani : wanafunzi 184 wapata ujauzito