Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohammed, amekanusha taarifa za uwepo wa Virusi vya Corona visiwani humo, kama ambavyo ilikuwa ikiripotiwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari za kujikinga na virusi hivyo.

Kauli hiyo ameitoa leo Machi 6, 2020, wakati akizungumza na waandishi wa habari visiwani humo na kuzitaka mamlaka husika, kusitisha uingiaji wa ndege za wageni kutoka nchini Italia kwa kipindi hiki sambamba na tamasha la ‘full Moon party’ hadi Serikali itakapojipanga.

“Hapa Zanzibar hatuna ugonjwa wa Corona na upotoshwaji juu ya hizi taarifa naviomba vyombo husika viwachukulie hatua madhubuti kwa watu wanaotoa taarifa zisizo sahihi, kuna ndege zetu za watalii kutoka Italy, tunawaambia waache kuja sasa hivi” amesema Waziri Mohammed.

Aidha, amesema wamesitisha tamasha la ‘ Full Moon Party’ iliyokuwa ifanyike Kendwa mkoa wa Kaskazini Ungujakwa kwani ilikuwa na Wageni zaidi ya 1,000 wanaohudhuria hivyo ingesababisha mkusanyiko mkubwa wa watu sehemu moja.

Prof. Kabudi awasilisha ujumbe wa JPM kwa Trump
China: Serikali yapiga marufuku ulaji wa popo, Nyoka, kuzuia Corona