Waziri Mkuu wa Sudan, Abdullah Hamdok amenusurika kuuawa baada ya msafara wake kulengwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
Televisheni ya taifa ya Sudan imetangaza kuwa Hamdok amepelekwa katika eneo salama, mkurugenzi katika ofisi ya Hamdo, Ali Bakhit,amethibitisha kuwa kiongozi huyo yuko salama.
Hadi sasa hakuna mtu au kundi lolote ambalo limedai kuhusika na jaribio hilo la mauaji.
Hamdok aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa Sudan mwezi Agosti mwaka 2019, baada ya maandamano ya kudai demokrasia kulilazimisha jeshi kumuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu wa nchi hiyo, Omar al-Bashir na kukabidhi uongozi wa serikali kwa raia.
Kwa mujibu wa Shirika la Fedha Duniani, mfumuko wa bei umefika asilimia 60 na kiwango cha ukosefu wa ajira kwa mwaka 2019 kilikuwa asilimia 22.1. hayo yote yanajiri kwaka mmoja tangu kuondolewa madarakani kwa Al-Bashir.