Maelfu ya wanawake nchini Mexico wamepanga kubakia nyumbani na kutokwenda kazini au shuleni ili kuadhimisha ”Siku ya Bila Mwanamke,” saa chache baada ya idadi kubwa ya wanawake kujitokeza mitaani jana kupinga unyanyasaji wa kijinsia wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Maandamano hayo yanaashiria kuongeza mapambano ya wanawake wa Mexico kupinga ghasia na kutothaminiwa mwanamke nchini humo ambapo ni katika ya nchi hatari zaidi kwa wanawake duniani.

Takwimu za serikali zinaonyesha kuwa wanawake 3,825 waliuawa mwaka 2019, Hiyo inamaanisha kuwa wanawake 10 wanauwa kila siku nchini Mexico.

Maria de la Luz Estrada mratibu katika taasisi ya taifa inayofuatilia mauaji ya wananchi, amesema Mexico wako katika mzozo wa kibinaadamu kwa sababu ya idadi ya wanawake wanaouawa au wanaopotea.

Uganda: sheria za ubaguzi kwa wanawake jeshini zabadilishwa
DAR kukumbwa na uhaba wa maji siku mbili