Jeshi la Polisi Nchini Uganda limefanya mabadiliko kadhaa katika kuwatetea wanawake wakati wakisherehekea siku ya wananwake duniani ikiwemo kufuta salamu ya”Sir” kwenye vyeo vinavyoshikiliwa na wananwake.
Ambapo viongozi wa Jeshi wamelenga kushughulikia suala la ukosefu wa usawa wa kijinsia mara baada ya kubainika kwamba Askari wa kike wamekuwa wakivaa suruali ambazo zinatengenezwa kwa ajili ya Askari wa kiume.
Hata hivyo nchi hiyo imefuta maagizo ambayo yalitolewa mwaka 1984 yaliyowataka Maafisa wa kike kuomba ruhusa kutoka kwa Inspekta Jenerali pale walipotaka kuolewa na raia wa kawaida (wasio askari).
Ambapo marekebisho hayo mapya ndani ya Jeshi hilo yatalenga kuwasaidia wanawake kupata nafasi za juu za Uongozi kutokana na wengi wao kushika nafasi za chini kwa muda mrefu na pia kuongeza fursa kwa Wanawake kujiunga na Jeshi hilo.