Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema baada ya Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufanya kikao cha dharura, wameshauri vikao vyote vya ana kwa ana kusitishwa mpaka pale Ugonjwa wa Corona utakapodhibitiwa.
Hatua hii inachukuliwa ambapo Mkutano wa Baraza la Mawaziri utakaowashirikisha Mawaziri kutoa nchi zote 16 Wanachama wa SADC, ulitarajiwa kufanyika Machi 16 na 17 mwaka huu Jijini Dar es Salaam
Waziri Ummy amesema hata kama hakuna mgonjwa, wanaweka nguvu kubwa zaidi katika kukinga maambukizi hayo, hivyo mikutano yote itakayoendelea kuanzia sasa itafanyika kwa njia ya mtandao
Aidha, ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuweka vituo kwa ajili ya waathirika wa Corona na wanajenga Kituo cha kudumu katika Hospitali ya Mloganzila.
Katika hatua nyingine waziri Ummy amesema kuwa wanatambua jitihada kubwa zinazofanywa na China katika kupambana na ugonjwa huu sambamba na kulinda wananchi wa nchi za SADC waliopo china.