Kiungo wa Simba Clatous Chama amemuomba radhi kiungo fundi Feisal Salum ‘Fei Toto’ kufuatia tukio la kumkanyaga makusudi kwenye mchezo baina ya timu hizo uliopigwa uwanja wa Taifa Jumapili ya March 08
Chama amethibitisha kuwa aliongea na Feisal na akamuomba radhi mapema jana lakini pia akatumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuomba radhi mbele ya mashabiki ambao wengi wamekerwa na tukio hilo alilofanya ambalo halikuwa la kiungwana
“Bro Feisal najua tumeongea leo lakini naomba nikuombe radhi tena mbele ya mashabiki wa mpira.”
“Mpira ni burudani na sio uadui. Forgive me bro!,” ameandika Chama kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Kuomba radhi ni kutambua kosa na kulijutia hivyo bila shaka Fei Toto pamoja na mashabiki wa Yanga, wadau wa soka wamemsamehe
Hata hivyo huenda kiungo huyo kutoka Zambia, akakabiliwa na hatua za kinidhamu kutoka kwa shirikisho la Mpira nchini (TFF).