Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetengeneza Daftari la Kudumu litakalosajili watoa huduma za fedha nchi nzima, wakiwemo Mawakala wa fedha za simu na Bima kuanzia Julai 2020
Hayo yameibainishwa na Mkurugenzi wa mfumo wa malipo wa malipo ya taifa (FRS) wa BoT Bernard Dadi wakati akizungumzia mfumo huo kwenye mafunzo ya waandishi wa habari amesema daftari hilo litakuwa sululisho kwa watoa huduma wa fedha wasio halali.
Lengo ni kuondokana na tatizo la watoa huduma vishoka na ambapo ameelaza kuwa Utekelezaji wa usajili unafanywa kwa awamu mbili Awamu ya kwanza inaanza Machi hadi Aprili 2020 na awamu ya pili itaanza Mei hadi Juni 2020
Aidha amesema kuanzia Julai watoa huduma za fedha watakaofanya kazi, ni wale tu waliosajiliwa na kupewa namba ya utambulisho
”Baada ya utekelezaji wake mtoa huduma atapewa namba ya utambulisho ya kipekee iliyo katika mfumo wa QR code sasa hapa wale wasio halali au wanaofanya kazi kwa kuwaibia wateja watakoma maana tutakutambua kwa namba yako” amesema
Amebainisha wanaopaswa kusajiliwa Matawi ya Benki, Mawakala wa Benki, Mawakala wa Pesa kwa njia ya simu za mkononi, Wakala/Dalali wa Bima, Wakusanyaji wa malipo kwa njia ya Kadi (POS), Wakala wa Hisa za Masoko ya mitaji na dhamana na Maduka ya kubadilisha fedha
Pia, huduma za Bima katika Taasisi za kiafya kama vile hospitali, vituo vya afya na maduka ya dawa, Mashine za kutolea pesa (ATM), Taasisi ndogo za kifedha (MFI) na vyama vya akiba na kukopa (SACCOS)