Hukumu inayowakabili viongozi wa chadema imeanza kusomwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo machi 10,2020

Hukumu hiyo inasomwa katika mahakama ya mkazi namba moja idadi kubwa ya wanachama na wafuasi wa chama hicho wamezuiwa kuingia mahakamani na kutakiwa kukaa nje.

Hukumu hiyo inasomwa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Thomas Simba huku ulinzi ukiwa umeimarishwa.

Viongozi mbalimbali wa Chadema wamejitokeza kusikiliza kesi hiyo wakiwemo wabunge na wenyeviti wa kanda huku wengine ni kutoka vyama vingine vya upinzani akiwemo mshauri mkuu wa ACT-Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad.

Katika kesi hiyo namba 122 ya mwaka 2018 washtakiwa wanakabiliwa na mstaka 13 ikiwemo kula njama kufanya mikusanyiko isiyo halali kati ya Februari 1 na 16 ,2018

 

Dkt. Ndumbaro afanya mazungumzo na Mabalozi wa Uswisi na Palestina
Mawakala wa fedha za simu kubanwa