Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Palestina Nchini Mhe. Balozi Hamdi Mansour AbuAli Pamoja na Kaimu Balozi wa Uswisi nchini Bw. Leo Nascher, katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo wamekubaliana kuendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi hasa katika sekta ya uwekezaji wa kiwanda cha dawa na vifaa tiba pamoja na kilimo.

Katika hatua nyingine,Dkt. Ndumbaro na Kaimu Balozi wa Uswisi nchini Bw. Leo Nascher mazungumzo yao yalihusu maandalizi ya mpango mpya wa maendeleo wa mwaka 2021-2024 baina ya Tanzania na Uswisi yanayoendelea.

Mpango wa maendeleo uliopo unatarajiwa kufikia ukomo mwaka huu 2020 ambapo mpango mpya utajikita zaidi katika kuimarisha sekta ya afya, mazingira, utawala bora na kukuza ajira kwa vijana na wanawake nchini.

Masuala mengine yaliyojadiliwa yalihusu programu ya Ukuzaji Ujuzi wa Ajira nchini (Skills for Employment Tanzania) na shuguli zinazofanywa na NGOs za Uswisi zilizopo nchini.

Pia Kaimu Balozi huyo alieleza kuwa Uswisi itaendelea kusaidia mradi wa malaria na kuchangia fedha katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

Kwa upande wake Mhe. Dkt. Ndumbaro alisifu uhusiano baina ya nchi hizi mbili kwa kueleza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Uswisi katika kukuza zaidi mahusiano hayo.

Taifa Stars ya CHAN 2020, AFCON 2021 yatajwa
Hukumu kesi ya Viongozi wa Chadema yaanza kusomwa