Jeshi la Magereza limekanusha ukiukwaji wa haki za binadamu magerezani baada ya kauli zilizotolewa na viongozi wa Chama cha Demokarasia na Maendeleo (CHADEMA) walipotoka gerezani na kueleza kuwa mambo yanayofanyika ni utaratibu wa kawaida kwa wafungwa na mahabusu.

Baadhi ya kauli zilizotolewa na Viongozi wa CHADEMA  baada ya kutoka gerezani ni pamoja na mateso ndani ya gereza ambapo wafungwa wanaishi kama wanyama, kutokuwa na haki na madai ya kupimwa UKIMWI hadharani.

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi, Amina Kavilondo amesema jukumu la Magereza ni kuhakikisha Usalama na afya ya mfungwa husika na wafungwa wengine na mfungwa akiwa na tatizo atakuwa chini ya uangalizi zaidi kuliko wengine.

Hata hivyo amesema wao kama viongozi ambao ni Wabunge katika majimbo mbalimbali watumie nafasi yao kupita katika Magereza na kufanya ukaguzi na kuzungumzia changamoto hizo ambapo zitapata uzito na kupatiwa ufumbuzi zaidi kuliko kusubiri mpaka wawe wafungwa ndio watoe Kauli hizo.

 

Video: Mchawi wa timu asimulia "Nilitafuta Kaburi la 1995" Tuliwakuta WCB| Nikiwa Uchi wa Mnyama
Mahakama: Msigwa alitoka kwa faini ya Magufuli