Rais wa Afrika Kusini Cyrill Ramaphosa ametangaza siku 21 kuanzia alhamis wananchi wote kujifungia ndani ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya Covid 19 nchini humo.
Amesema kuwa wakati wa utekelezaji wa suala hilo linalotarajia kumalizika Aprili 16 hakuna mtu yeyote atakaeruhusiwa kutoka nyumbani na watakosimamia jambo hilo ni idara ya Maafa ya nchi hiyo.
Hadi asubuhu ya leo Machi 24, 2020 tayari nchi hiyo imeripoti maambukizi 402 huku kukiwa na wagonjwa wanne waliopona ugonjwa huo wa Corona.
Katazo hilo la watu kutoka ndani halitawahusu watu wa Idara ya Majanga, Polisi na Watumishi wa Afya watakaokuwa wakizunguka kwa wananchi kuwapatia mahitaji muhimu pamoja na chakula.