Familia zinazokadiriwa kuwa na watu 90 zimekimbia nyuma zao baada ya ziwa Tanganyika kujaa maji na kusababisha mafuriko.
Imeelezwa kuwa takribani nyumba 18 zilizojengwa maeneo ambayo awali ziwa Tanganyika lilikuwa linafika kijiji cha Kirando wilayani Nkasi zimejaa maji.
Diwani wa kata ya Kirando, Kakuli Seba ameliambia gazeti la Habari leo kuwa maji ya ziwa Tanganyika yamefika maeneo lililokuwa miaka 30 iliyopita na kusababisha mafuriko.
Ameopngeza kuwa miongoni mwa nyumba zilizozingirwa na maji ni pamoja na hoteli pamoja na kituo cha mafuta.
“Hoteli ya Nkondwe Beach imefurika maji jana na imelazimika kufungwa. Yaani ukiacha milango wazi samaki wanaingia chumbani….unaweza kuwavua. Pia biashara ya samaki imekuwa ngumu baada ya mwalo wa samaki kufurika maji” Ameeleza Diwani Seba.