Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amehalalisha upikaji na unywaji Gongo inayotengenezwa kwa Mabibo kwani ni salama kwa matumizi ya binadamu.
Ameeleza kuwa baada ya kupeleka sampuli za Gongo hiyo kwa mkemia mkuu wa Serikali majibu yametoka kuwa haina madhara.
Pia amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mtwara kuwasajili wapika Gongo wote ndani ya miezi 2 na polisi kuacha mara moja kuwakamata wapika na wanywaji Gongo ya mabibo.
Aidha, amemwandikia Waziri wa Katiba na sheria kuanza mchakato wa kubadilisha sheria ili kuhalalisha gongo ya mabibo.
Pia amemwandikia Waziri wa viwanda na biashara kutafuta wawekezaji ili waende Mtwara kujenga viwanda vya spirit na sanitizer kwa kutumia Mabibo.