Katika visiwa vya Maurutius, kuanzia Aprili 2, maduka na Supermarkets zitafunguliwa kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni na zitahudumia kwa sheria zote za usafi ili kupunguza maambukizi. Pia manunuzi yatafuata herufi za majina ya familia
Jumatatu na Alhamis, watahudumiwa wenye herufi A hadi F, Jumanne na Ijumaa watahudumiwa wenye herufi G hadi N, Jumatano na Jumamosi watahudumiwa wenye herufi O-Z.
Imeelezwa kuwa wenye kufanya ununuzi mtu anatakiwa kuwa na kitambulisho cha Taifa, kwa wageni watatumia passport, mtu mmoja ataiwakilisha familia na atatakiwa kuvaa barakoa, atafanya ‘shopping’ kwa dakika 30 tu.
Pia ununuzi wa vitu unadhibitiwa ili mtu asinunue vingi kwa kuhodhi. Mfano, mtu ataruhusiwa kununua ‘toilet papers’ 3 tu kwa kila mtu mmoja
Mpaka sasa nchi hiyo imethibitisha kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona kwa watu 161 huku vifo vikifikia watu 6.
Serikali ya Mauritius imeongeza muda wa kubaki ndani ili kujiepusha na janga hilo ambapo raia watabaki ndani hadi Aprili 15.