Waziri mkuu, Kassim Majaliwa leo Aprili 8,2020, ametoa wito kwa wananchi katika kuendelea kuepuka mikosanyiko isiyoyalazima wanaweza kuanza na kuepuka mikusanyiko ya sherehe za harusi kwani sio muhimu sana kufanyika kwa muda huu wa mlipuko wa virusi vya covid 19 duniani, ambapo Tanzania inawagonjwa 25.
Amebainisha hayo alipokuwa akipokea michango kutoka kwa wadau mbalimbali kwaajili ya kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na ugonjwa wa Corona, kwenye Viwanja vya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa Dodoma.
“Kufunga harusi kwa sasa sio muhimu sana watu wajiepushe, tunajua kuna maeneo nyeti kwenye maduka, Hospitali, masoko kwa lengo la kupata huduma, wanaoenda huko wazingatie umbali kutoka Mtu mmoja hadi mwingine, tunajua Watanzania wengi tunaishi kwa kupata leo na kula leo tukizuia moja kwa moja tunaweza kutengeneza tafrani ya hali ya juu” Amesema Waziri mkuu.
Katika michango hiyo amepokea hundi ya sh. 1,000,000,000/= kutoka kwa Mfanyabiashara, Rostam Aziz ukiwa ni mchango binafsi wa mfanyabiashara huyo wa kuunga mkono mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID – 19.
Amepokea lita 50,000 za mafuta kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah.
Halikadharika Waziri mkuu, amepokea hundi ya Sh. 79,000,000/= ukiwa ni mchango wa ASASI za Kiraia,na hundi ya sh. 4, 000,000,000/= kutoka kwa kampuni ya madini ya Barric – Twiga Minerals, iliyowasilishwa ba Meneja Mkazi (Country Manager) Hilaire Diarra.