Rais wa Iraq Barham Saleh amemteuwa mkuu wa ujasusi, Mustafa Kadhemi kuwa waziri mkuu mpya wa tatu wa nchi hiyo ndani ya mwaka huu 2020.
Hafla ya uteuzi huo ilihudhuriwa na vigogo wakuu wa kisiasa nchini humo, kuashiria uungwaji mkono mkubwa wa Kadhemi ambao mawaziri wawili waliokuwa wameteuliwa hapo awali hawakupewa.
Kadhemi, ambaye ni mkuu wa Idara ya Kitaifa ya Ujasusi mwenye umri wa miaka 53, kwa muda mrefu amekuwa na mahusiano ya karibu na Marekani lakini duru za kisiasa zinasema pia ana mahusiano yaliyoimarika na adui wa Marekani, Iran.
Mwenzi uliopita waziri mkuu aliyekuwa ameteuliwa alijiuzulu bofya hapa kufahamu zaidi Waziri mkuu Iraq ajiuzulu.