Meneja wa kikosi cha Chelsea, Frank Lampard, amekiri anahitaji kukiimarisha zaidi kikosi chake ili aweze kushindana na Liverpool na Manchester City katika ubingwa wa EPL.

Lampard, hajafanya usajili wowote mkubwa tangu ajiunge na Chelsea mwanzoni mwa msimu huu, lakini timu yake ipo ndani ya nne bora kwenye msimamo wa EPL, japokuwa ameachwa pointi 34 na vinara Liverpool.

Akizungumzia muelekeo wa kikosi chake kwa msimu ujao wa mashindano, Lampard, amekiri kuwa anahitaji kuendelea kujijenga na kusajili nyota kadhaa wapya ambao wataongeza ushindani.

Wakati huo huo, maisha ya nyota wa Argentina, Mauro Icardi ndani ya Inter Milan, huenda yakafikia ukingoni msimu huu, baada ya Makamu wa Rais wa timu hiyo, Javier Zanetti, kudai kuwa hadhani kama nyota huyo ana maisha tena ndani ya Inter.

Icardi aliingia kwenye mgogoro na viongozi wa Inter Milan pamoja na mashabiki mwaka jana, jambo ambalo lilisababisha apokonywe unahodha na kupelekwa kwa mkopo PSG ya Ufaransa.

Inaelezwa kuwa huenda PSG ikamsaini staa huyo moja kwa moja baada ya kuifungia timu hiyo magoli 20 na pasi nne za magoli katika mechi 31 alizocheza msimu huu.

Mabingwa wa Italia, Juventus wanatajwa kuwania saini ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 27, na tayari mke wake, Wanda amedai kuwa wanaweza kurejea Italia.

Senzo Mazingisa atangaza vita
Clatous Chama ajilipua, aweka hadharani kila kitu