Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mazingisa ameshangazwa na makamu mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Fredrick Mwakalebela kusema kuwa klabu hiyo imeanza mazungumzo na Clatous Chama.

Jana Jumatatu Mwakalebela alizungumza na vyombo vya habari na kueleza kuwa, Young Africans imeanza mazungumzo na nyota huyo kutoka nchini Zambia, kwa kigezo cha kuwa na mkataba chini ya miezi sita na Simba SC.

Senzo amesema kama Fredirick Mwakalebela alikuwa anaongea kuwafurahisha mashabiki wake itamutokea puani.

Afisa mtendaji huyo wa Simba SC CEO amedai kuwa atapambana na kiongozi huyo wa Young Africans ili wajue namna ya kuendesha mpira na kuacha mambo ya ubabaishaji na siasa kwenye mpira.

Pia Senzo ameshangaa kuona kiongozi mkubwa wa Young Africans akiongea kwenye vyombo vya habari bila wasiwasi akijadai ameongea na Chama, kitendo ambacho ni kosa kubwa.

“Kutangaza kwenye vyombo vya habari umeongea na mchezaji ambaye ana mkataba na Klabu yake huo ni ushahidi tosha wa kumshitaki mtu/klabu kokote.”

Hata hivyo tayari Chama ameshakanusha kuzungumza na uongozi wa Young Africans na kubainisha kuwa, ataendelea kuitumikia Simba SC kutokana na mkataba uliopo baina yake na klabu hiyo iliyomsajili akitokea Lusaka Dynamos mwaka 2018.

Mwakalebela asalimu amri na kuomba radhi
Lamprad atangaza hali ya hatari, Icardi hatarini kuondoka Inter Milan