Mbunge wa Iramba (CCM), Mwigulu Nchemba, amesema viongozi wanatakiwa wawe na kauli moja wasifanye siasa katika ugonjwa wa virusi vya Corona.
Amesema kuwa lugha ya kwanza ambayo inatoka kwa viongozi ni kujikinga na maaambukizi ya virusi vya Corona.
“Watanzania kila mmoja achukue hatua katika jambo hili mimi nilivyokuwa nawaza hata taarifa tunazozitoa zibaki za aina tatu tu ya kwanza iwe inaeleza huu ugonjwa bado upo, ya watu waliopona na waliokufa” alisema Nchemba.
“Tunavyoongea kila wakati kuonyesha kwamba serikali hakuna jambo walilofanya ni kuwapoteza watu wetu sikiliza lugha nyingine utakuta watu wanazungumza mabasi yanajaa, bado tunapitia madirishani unamuambia nani? Hivi kweli serikali ikutafutie basi la kuondoka au ikutafutie polisi kuzuia kila mmoja asipite dirishani,” amesema
Katika hatua nyingine amesema kuwa suala la kutangaza kuongezeka wagonjwa halijakaa sawa na hajui ni kwani kuna baadhi ya watu wanatamani takwimu iwe kubwa na kutamani wagonjwa kuwa wengi.