Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, dkt. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa watu 18 waliopoteza maisha katika ajali iliyotokea leo Aprili 15, 2020 , saa 12 : 55 asubuhi katika kijiji cha Kilimahewa Kaskazini, Mkuranga mkoani Pwani.


Rais Magufuli amemtaka mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kufikisha salamu zake kwa familia za marahemu na ameeleza kuwa anaungana nao katika kipindi hiki cha majinzi ya kuondokewa na wapendwa wao.


” Nawaombea familia za marehemu wote, ndugu, jamaa na marafiki kuwa na moyo wa uvumilivu na usatahimilivu katika kipindi hiki kigumu caha majonzi, kuwapoteza watanzania wenzetu kwa idadi kubwa kuama hii inaumiza sana” Amesema Rais Magufuli.


Aidha amevitaka vyombo vya usalama barabarani kuhakikisha vinachukua hatua madhubuti za kuzuia ajali za barabarani na amewataka madereva na wote wanaotumia barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali ambazo zinagharimu maisha ya watu na uharibifu wa mali.

Barakoa lazima kwa wahudumu wa baa
Simba SC yamkalia kooni Mwakalebela