Mabingwa wa soka Tanzania bara Simba SC, ndiyo klabu pekee kutoka ukanda wa Afrika mashariki na kati kuwemo katika orodha ya vilabu 10 bora vinavyoongoza kwa wafuasi kupitia mitandao ya kijamii (wafuasi 2M).

Kwa mujibu wa mtandao wa Digital Sports Africa, wafuasi hao wametoka katika mitandao ya Instagram, Facebook, Twitter, YouTube, TikTok na linkedin, ambapo klabu ya Al Ahly ya nchini Misri inaongoza ikiwa na wafuasi milioni 27, ikifuatiwa na Zamalek SC yenye wafuasi milioni 12 na Raja Club Athletics ya Morocco ikishika nafasi ya tatu kwa wafuasi milioni 6.

Klabu ya Azam FC inakamata nafasi ya 13 katika listi hiyo ikiwa na wafuasi takribani wafuasi milioni 1 na klabu ya Yanga 957,000.

Kampuni ya Digital Sports Africa  ambayo ni sehemu ya mtandao wa Realsport ya Ujerumani, mgawanyo wa 10 bora kikanda uko hivi.

  • Vilabu 7 – ukanda wa Kaskazini (Misri, Tunisia, Morocco).
  • Vilabu 2 – ukanda wa kusini mwa Afrika (Afrika Kusini).
  • Klabu 1 – ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (Tanzania).

Bongani Zungu alivyoshindwa kulipa fadhila
Sakata la Clatous Chama latua TFF