Serikali inatarajia kuajiri watumishi wapya 44,811 akiwemo wa kada ya elimu 13, 529 na afya watumishi 10, 467 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020/21 upande wa ajira za watumishi wa umma.

Akiwasilisha bajeti ya ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, jijini Dodoma kwa njia ya video kutoka ukumbi wa Msekwa na ukumbi wa bunge, waziri George Mkuchika amesema watumishi hao watasaidia kuongeza ajira nchini.

Wengine wataajiriwa katika kilimo, mifugo na uvuvi ambao ni 2, 145, Magereza 685, Uhamiaji 495 na hospitali za mashirika ya kidini na hiari zitaajiri wafanyakazi 1, 262.

Waziri mkuchika amesema pia wizara inatarajia kupandisha vyeo watumishi 222, 290 wa kada mbalimbali kulingana na maelekezo yaliyotolewa.

Pia serikali inatarajia kuajiri watumishi 13, 002 wa kada nyinginezo wakiwemo wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma nchini.

Halikadharika wizara itaendelea kuchambua na kuhakiki madai ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa umma 20, 027 yanye thamani ya bilioni 45.74.

Mwanza: Wafungwa wauawa wakitoroka gerezani
Wagonjwa wa COVID 19 Wafika 88 Tanzania.